Tag

kitukuzwe


Browsing

Mwandishi:Sultan Karama Maji Male (kero)

Naam,ninaposhika kalamu kwa Mara nyengine tena, mara hii siandiki shairi kama ilivyo ada yangu bali ni kutafakari. Ni kutafakari tafakuri la sauti ili wasomaji nao wapate kutafakari na Mimi. Suala la uboreshaji was lugha ya kiswahili limepewa kisogo na muluki ya watu,sio kuwa wengi hawajui kiswahili Ila tu ni ile dhana iliotawala bongo zao ya kuwa kiengereza ni bora. Halikadhalika ni unasibishwaji wa lugha ya kiengereza na usomi.

Dhana ya kunasibisha lugha ya kiengereza na usomi ndicho chanzo kikuu cha kusambaratisha juhudi za wakereketwa wa lugha ya kiswahili katika kuikuza lugha hii. 

Stesheni za runinga na redio pia zimelemaa katika kuboresha lugha hii. Pindi nilipokuwa mdogo kulikuwa na vipindi maridadi kabisa vikiwemo:KISWAHILI KITUKUZWE KWANI NI LUGHA YA TAIFA. Ila ni kwa masikitiko makuu Taifa la Kenya limekuwa taifa lililo sahau chimbuko lake. Limekuwa taifa linalobeza tamaduni zake na kutupilia mbali turathi zake.  Waama tumesahau kuwa muacha mila ni mtumwa. Tamati ningependa kuwashajiisha katika kukienzi kiswahili. Kiswahili kitukuzwe kwani ni lugha ya taifa.